KUMSIKIA MUNGU

kumuona

Hatuwezi kisikia ikiwa hakuna kinachoongelewa. Kusikia sauti ya Mungu means Mungu anaongea. Kuna tofauti ya kusikia na kusikiliza (Listen means to pay attention to a sound or speech... Hear means to perceive, to acknowledge a sound.) Unaweza kusikiliza lakini usisikie. Thus why title inatuambia kusikia sio kusikiliza sauti ya MUNGU. Katika hi duniani sio kila anayesikiliza anasikia Ndio maana mnaweza kuwa katika darasa moja mkamsikiliza Mwalimu lakini kila mtu akasikia la kwake na wakati mwingine hata usisikie.

Mambo mengi duniani ni matokeo ya kusikia sauti. Hata utiifu ni matokeo ya kusikia sauti. Huwezi kutii kama hujasikia

Mungu anaongea nyakati zote lakini sio watu wote humsikia. Kutokumsikia Mungu haina maana kua Mungu haongei

Mathayo 13:15
Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

1 Wakorintho 2:9 
lakini, kama ilivyoandikwa, mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.

Mungu ndiye aliyeniumba, namna ya kuishi kwangu yategemea sauti yake. Siwezi kuyaishi maisha kwa kutegemea akili yangu maana sio Mimi niliyejiumba, nimeumbwa.

Sauti ya Mungu imebeba maelekezo ya namna gani niishi, namna gani nitembee.
Hatuwezi kumtii Mungu kama hatumsikii. Kutii ni matokeo ya kusikia. Huwezi kutii usichokisikia.

Hatujajiumba, tumeumbwa hivyo mmiliki wa maisha yetu ni MUNGU mwenyewe. Kushindwa kusikia yeye ni chanzo cha kuelekea uharibifu na uangamivu.

Kama ilivyokua kwa anayetengeneza pasi anakua amelenga pasi itumike kwaajili ya kunyooshea nguo na anayetengeneza heater amelenga kwaajili ya kuchemshia maji. Hivyo kabla hujaanza kutumia vifaa lazima upate instruction/menu/maelekezo toka kwa manufacturer ambayo itakuonesha
How to use it
Muda wa bidhaa hiyo kudumu
Expire date
Inayoonesha warning. Inayokuonesha mambo ambayo yanaweza tokea ikiwa bidhaa hiyo itatumika kinyume na maelekezo.
Cha kushangaza katika ulimwengu huu wachache sana husoma menu (instruction) kabla ya matumizi. Swali dogo hata uliponunua simu yako je ulishasoma kile Kitabu cha maelekezo?! Kutokujua maelekezo kunaweza kukupelekea kuitumia ile bidhaa kinyume na dhumuni husika. Kutokusoma maelekezo unaweza kutoa katika mambo 40 ambayo bidhaa hiyo imeandikwa kutumika kwayo unayajua machache tu.

Same apply to our life, watu wanazaliwa wanaishi lakini hawana instruction za wamezaliwa kufanya nini.
Hakuna kitu hatari kama kutokusikia sauti ya Mungu. Dhambi ni matokeo ya kutoisikia sauti ya Mungu. Kutokusikiliza sauti ya Mungu kinaweza kukupeleka mtu kwenye mauti na uharibifu.

MUNGU BAADA TU YA KUMUWEKA MWANADAMU ADAMU ALIMPA INSTRUCTION

Mungu alimuweka huyu Binadamu Edeni. Nilikua na maeneo mengi but why alikuweka Edeni?

Mwanzo 2:7-8
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

Mungu alitoa resources/materials for Adamu Mwanzo 2:9-11.

Mungu anampa maagizo ya namna imempasa adamu kuishi. Mwanzo 2:16-17
Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mungu anampa instruction Adamu.
Anamwambia nini Afanye
Anamwambia nini Asifanye
Anamwambia yatakayotokea ikiwa atakiuka hayo maagizo.

Pamoja na Mungu kumpa Adamu instruction zote bado suala la maamuzi lilibaki kwa Adamu. Na tunaona baadae baada ya Adamu kwenda kinyume nini kilitokea.
Bidhaa ikitumika kinyume na maelekezo ya manufacture lazima tu iharibike.

The same apply kwa bidhaa za dukani. Uki violate rules Basi unaelekea uharibifu. Whether umesoma instruction au hujasoma. Hata kama hujui kuwa simu ikiwekwa kwenye maji huharibika siku ukiiweka huharibika. Kutokujua au kujua hakuzuii bidhaa kuharibika ikiwa imetumika kinyume na lengo husika.

Mungu anapokupeleka eneo lolote tamani sana kujua maelekezo toka kwake. Musa pamoja na kwamba wanaenda kanani nchi nzuri yenye asali lakini bado alimwambia Mungu usipoenda nasi hatuwezi kutoka hapa. On other way anamwambia bila sauti yako hatuwezi kutoka hapa.

Kutoka 33:15
Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.
And he said unto him, if thy presence go not with me, carry us not up hence.

Sauti ya Mungu ni Mungu mwenyewe, Uso wa Mungu ni Mungu mwenyewe. Kama huna maelekezo ya hatua nyingine unayoiendea ni bora kuto kwenda mpaka umesikia sauti ya Mungu.

Kuna maeneo Mungu anaweza kukupeleka, kuna nafasi ambazo Mungu anaweza kukupeleka kwa kusudi. Kuna vyeo, kuna ofisi unapelekwa kwa kusudi, kama hutakua making kusikia sauti ya Mungu ni rahisi kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

Esta angeweza kujisahau kuwa alikua malkia kwa wakati ule ili tu kuwakomboa wayahudi wakati ule wa maangamivu Basi wayahudi wangeangamia.

Esta 4:13
Naye Mordekai akawaagiza wampelekee Esta jibu la kusema, Wewe usijidhanie kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote.Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?

Mungu anapokuweka eneo tamani sana kutaka instruction toka kwa Mungu regardless of the experience you have. Maisha ya mwanadamu yamebebwa na instruction (ambayo ni sauti ya Mungu).

HOW GOD SPEAK.
Mungu ni Roho, Namna anayoitumia kuongea na watu wake ni kwa namna ya Roho. Ni Mara moja katika Bible Mungu alishuka na kuongea na Musa. Hakuna mwanadamu anayeweza kumuona Mungu akaishi, Mungu mwenyewe sababu utukufu wake hauchangamani.
Kuna namna nyingi ambazo Mungu huzungumza. Kutokumsikia Mungu haina maana kuwa Mungu haongei. Mungu anaongea though sio kila mtu humsikia.

1: Njozi na maono
Kuna njozi zinakuja kwa sababu ya uchovu .
Mhubiri 5:3
Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.

Kuna njozi adui huzileta 
Yeremia 23:25,27.
Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.

Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali. 

Kuna ndoto zitokazo kwa Mungu kukufikishia ujumbe.

Mwanzo 20:3
Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.

Mwanzo 31:10-13
Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa.

Kwa njia ya ndoto Mungu anaweza kukuonya.

Mwanzo 31:24
Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

Mathayo 2:12
Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.

Mungu hutumia ndoto kukupasha habari kuhusu mambo ya siku za usoni (your future).
Waamuzi 7:13 na 15
Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini.

Ikawa, aliposikia habari ya ile ndoto, na kufasiriwa kwake, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana Bwana amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu.

Mwanzo 37:5
Yusufu akaota ndoto, akawapa ndugu zake habari, nao wakazidi kumchukia;

Mungu kutumia ndoto kukufariji.
Mwanzo 15:1
Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.

Kuna majibu MUNGU huachilia kupitia njozi

1 Falme 5:5, 15
Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.

Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la agano la Bwana, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.

2: Watumishi wake.
Eliya na Ahabu.

1 Falme 21:17-19
Neno la Bwana likamjia Eliya Mtishbi, kusema, Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. Ukamwambie, ukisema, Bwana asema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki? Nawe utamwambia, kusema, Bwana asema hivi, Mahali pale mbwa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.

3: Kwa njia yabFikra/Mawazo ndani ya Moyo kupitia Roho Mtakatifu.

NOTE.
Unahitaji Neno la Mungu ili kuzipambanua instruction zote hapo juu.
Instruction zote za namna gani mwanadamu aishi IPO kwenye NENO.
Na NENO ni Mungu mwenyewe. Neno ndio menu ya MTU uishije. Sauti ya Mungu IPO kwenye Neno la Mungu. 

Kadiri unasoma Neno linafanyika akiba na majibu hata utakapoona kuchoka. Neno la MUNGU ni sauti ya Mungu Mwenyewe. Neno la Mungu halikai kwenye akili, halikai kwenye miguu. Neno la Mungu linakaa moyoni.  Kadiri unalisikia Neno unasikia Mungu mwenyewe. 

Zaburi 119:11
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.

Ikiwa Dhambi ni matokeo ya kutokusikia, na Neno ni sauti ya Mungu mwenyewe hivyo, kutokuliweka Neno ndani ya Moyo (kutokumsikia sauti ya Mungu) kunampelekea mtu kutenda dhambi. (Dhambi ni uasi, kutumika kinyume na lengo husika)

Na dhambi ikikomaa inasababisha mauti, thus why Neno la sema 

Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Katika ulimwengu tunaoishi kuna sauti nyingi.
 Sauti za marafiki, za wazazi, za watumishi, za maadui etc.

Sauti zote hizo ili kuzichambua wahitaji kuwa na Neno ndani na mahusiano ya kudumu na Roho Mtakatifu.

Sio wakati wote ambao Mungu anaweza kutumia mtumishi wa Mungu. Adui pia hutumia.
Hebu Tujifunze kwa Petro. 

Mathayo 16:17-19
Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.

Marko 8:33 (from 27)
Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

Tunaona Petro yule yule ambaye alipata mafunuo ya ki Mungu sasa adui anamtumia kuongea ufunuo usio wa Ki Mungu. Unahitaji sana Msaada wa Roho Mtakatifu kuzichambua sauti. Kigezo cha kuwa mtumishi wa Mungu sio guarantee ya kuamini kila anachosema.. You need Holy Spirit kuchanganua na Neno la Mungu.

Mtumishi pia anaweza kuwa kama limitation kuzifikia hatua nyingine.
Tu angalia kipindi Yesu anabatizwa.

Mathayo 3:13-17
Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe.
Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Yohana anataka kumzuia Yesu kubatizwa na kujiona hastahili kumbatiza. Kuna wakati ni muhimu na ni lazima utii sauti ya Mungu hata kama umeelekezwa kwa watu ambao ki cheo au umri ni wadogo kuliko wewe.

Eliya na Elisha.
2 Falme 2:1-15.

MADHARA YA KUTOKUSIKIA SAUTI YA MUNGU.
1: Yanakupelekea mauti.
Unaposhindwa kusikia sauti ya Mungu unafungua mlango wa mauti, sio mauti ya kimwili pekee Ila na mauti ya Kiroho. 1 Falme 13:1-20.

Shetani Mara zote hujigeuza kuwa Malaika wa Nuru.

 2 Wakorintho 11:4
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

2: kutokufanikiwa.
Mafanikio yamefichwa kwenye kusikia sauti ya Mungu. 

Isaya 1:19
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

3: Kuondolewa  kwenye nafasi Mungu aliyokupa.
Isaya 66:2
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.

1 Samweli 15:22 (1-28)
Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

1 Samweli 16:14
Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. 

Sio mazingira yote huwa mepesi kutii sauti ya Mungu lakini katika hali hiyo hiyo ni lazima kukubali kutii ... Kina Daniel wanakubali kutii sauti ya Mungu ya kutokuibudu wala kuisujudia miungu mingine na matokeo yake wanatupwa kwenye tundu la simba na kwenye tanuru la moto.
Kuna wakati unaweza hata kuhatarisha maisha yako katika kutii sauti ya Mungu..

4: Ardhi yaweza kulaaniwa kwa watu kutosikia na kutii sauti ya Mungu.
Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

MAMBO GANI YANAWEZA KUKUPELEKEA KUTOKUSIKILIZA SAUTI YA MUNGU?

1: Kutokuwa na mahusiano ya kudumu mtu pamoja na Mungu

Yohana 10:4-5
Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.

2: Kukosa ufahamu juu ya Neno.
Zaburi 23:1-2
Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3: Taarifa zipi unapenda kuzisikia?
Kukosa utulivu wa ndani 

No comments