Mfanye MUNGU Kuwa Kipaumbele Chako cha Kwanza 'Make GOD Your First Priority'Umeanzaje mwaka 2020? Ni swali ambalo ningependa kuanza nalo pindi usomapo chapisho hili, ikiwa  tunazidi kusonga mbele katika mwaka mpya 2020 huku siku zikiwa bado ni mpya kabisa... Tuanzie hapa => Mara nyingi watu wengi pindi tukikwama ndio huanza kukumbuka kumbe yupo MUNGU asiyeshindwa lakini tunapoanza huwa hatukumbuki kuwa yupo MUNGU asiyeshindwa tunaanza mipango na mambo yetu wenyewe huku tukimuweka MUNGU pembeni.

Ni dhahiri kuwa LAZIMA unapoanza mwaka uwe na VIPAUMBELE katika malengo yako yaani Yale mambo muhimu ambayo unatamani kuyakamilisha kabla ya mengine. Ndio vipaumbele ni muhimu sana lakini ili ufanikiwe unamuhitaji MUNGU zaidi katika safari yako ya mwaka 2020. Katika mipango yako yote ni muhimu kwa MUNGU kuchukua nafasi ya kwanza (Namba moja)

Tunajifunza sana hasa kwa wana wa-Israel KUTOKA 33:15 Katika safari yao walipomkosea MUNGU na MUNGU akakataa kwenda nao maana aliogopa hasira yake isijewaangamiza Mussa alipogundua bila MUNGU safari yao isingekua salama, wasingefika mwisho na akaamua kukataa kwenda bila uso wa MUNGU yaani uwepo wake, ndio wangeweza kwenda bila MUNGU lakini wasingefika safarini salama, ndivyo wengi huwa tuko tayari kwenda na mipango yetu na kumuacha MUNGU ila tukikwama tunarudi kwake yaani tunamfanya MUNGU ziada na wamaana pale mambo yanapoharibika.

Hitimisho:Huwezi kuanza bila Mungu na ukataka umalize na Mungu, Huwezi kumaliza na Mungu kama hukuanza na Mungu...2020 ni mwaka wa kuinuliwa kwako.

No comments