Mfahamu Reinhard Bonnke: Muhubiri aliyetikisa dunia

Muhubiri Reinhard Bonnke, enzi za uhai wake

Shalom wapendwa katika Bwana, ni matumaini yetu kuwa mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku.


Moja kwa kwa moja leo naomba tukumbushane kidogo kuhusu mtumishi wa Mungu aliyewahi kuvuma sana hapa Duniani enzi za miaka ya 1970 - 2003, Mtumishi kutoka Ujerumani aliyejulikana kwa jina la REINHARD BONNKE.

Alizaliwa mwaka 1940-4-19. Alimpokea YESU akiwa na miaka 9 kwenye mkutano uliofanywa na huko MUNICH mwaka 1949 akiwa ndie mtoto pekee aliyenyoosha mkono na kuhitaji kuokoka. Baada ya kuokoka alikuwa na kipaji cha kipekee cha kuchambua vitabu vya dini hadi wazazi wake walitamani akasomee ukasisi na baadaye aje kuwa papa lakini haikuwezekana.

Akiwa na miaka 17 aliandika kitabu cha “Time is running”. Alijunga na masomo ya Bible School huko Swansea.

Bonnke alioa mwaka 1964 akapata wototo 3 na wajukuu 8

Mwaka 1974 Bonke alianza huduma yake akiwa na watu 100 hivi, baadaye 1986 alianzisha  chama cha CHRIST FOR ALL NATION “CfaN” 

Bonnke alizunguka zaidi ya nchi zote Afrika ikiwemo Tanzania, katika mikoa ya Dar es Salaam na Kilimanjaro

NIGERIA
SOUTH AFRICA
UGANDA
KENYA
UGANDA
DRC
NIGER
ZAMBIA
MALAWI

Na nchi nyingine nyingi hapa na Duniani; huku akishika nafasi ya juu kwa kuweza kukusanya watu kwenye mikutano yake ambayo wahudhuriaji wa mikutano yake hawakuwa chini ya Laki 4. 

Bonnke alifariki wikiendi iliyopita (Dec 7, 2019) akiwa na umri wa miaka 79.

Anajulikana kama ''GREAT AFRICAN MISSIONARY'' Ameacha alama kubwa sana Duniani tangu miaka ya 1990 hadi leo hakuibuka mtu wakujaza nafasi kama yake katika mikutano aliyowahi kuifanya Afrika na Dunia kwa ujumla.

Kwa ufupi tumekumbushana tu juu ya BWANA REINHARD BONNKE muhubiri aliwahi kuitikisa Dunia.

No comments