Fred Msungu: 'UTATA WA TAREHE, SALAMU YA CHRISTMAS'


KWA NEEMA YA MUNGU TUMEFIKA MAJIRA HAYA TENA KHERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA 2020...Neema ya Mungu iliyotufikisha hapa...neema hiyo hiyo inauwezo wa kutuvusha...kwa neema ya Mungu tutavuka salama kuelekea 2020

(▪️Sehemu ya pili▪️) Kumekua na mijadala na mitazamo juu ya tarehe 25...kwanini / wengine wanarejea kwenye asili ya sikukuu iliokua inafanyika tarehe hizo....na kusema si halali kusherekea kwasababu ilikua sherehe ya kipagani, Wengine mijadala yao wameiweka kwa ( Santa clouds) a.k.a babu Christmas.....
Mitazamo binafsi imekua mingi kila mtu na anachokiona kuwa sawa.......Miaka 300 Baada ya Kristo ndio sherehe hii ilianza kuadhimishwa na kutokea hapo imekua mpaka sasa.... ni kweli kunaweza kuwa na mitazamo mingi na maana tofauti za majina/ ishara asili ya tarehe na mambo yaliowahi kufanyika awali.....lakini kwetu sisi hizo sio habari muhimu ..kwasababu kimsingi ukitaka kufuatilia kila kitu na siku yake na kilianzaje inawezekana hakuna utakalolifanya maana Sikh zenyewe ziko 7 tu ....na zote zilishawahi kutumiwa awali kwa matumizi mabaya na mazuri kulingana na nia za watu husika ......sasa tufanyaje ? 🎯 Jambo muhimu hapa sisi kwetu sio asili ya tarehe , wala kitu gani kitu gani kilifanyika....JAMBO LA MSINGI KWETU TUNACHOKIJUA
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Kwetu hili ndio la muhimu zaidi na ndio sababu ya kusherekea kwetu .HATUISHEREKEI SIKU ( tarehe ) TUNAMSHEREKEA BWANA WA SIKUSource: Fred Msungu IG Page

No comments