PASTOR SAFARI PAUL: USHAURI KWA WATUMISHI WAIMBAJI NA WAPIGA VYOMBO VYA MUZIKI


Wiki kadhaa zilizopita niliandika na kutoa ushauri kwa watumishi WACHUNGAJI, WAINJILISTI, WALIMU, MITUME NA MANABII kuhusu kumuabudu Mungu wakiwa kwenye Ibada.
Leo naandika kwaajili ya waimbaji na wapiga vyombo wanaotumika madhabahuni.


USHAURI
1. TUJIFUNZE KUMWABUDU MUNGU TUKIWA KWENYE IBADA
• Huduma yetu ya kwanza siyo kuwahudumia watu bali ni kumuhudumia Mungu. Sisi ni ukuhani wa Kifalme na wito wetu wa kwanza ni kumtolea Mungu dhabihu za kiroho 1 Petro 2:5,9 .
• Tunapokuwa kwenye Ibada tumwabudu Mungu pia tukae kwenye IBADA mpaka mwisho tuhudumiwe.
- Baadhi ya waimbaji , wapiga vyombo (Wanamziki) hawakai kwenye Ibada. Wakishuka kutoka madhabahuni wanatoka nje au wanakuwa busy na simu zao. Kutii ni bora kuliko dhabihu. 1 Samuel 15:22. Mungu hanashida na huduma yako kwanza, Mungu anataka moyo wako. Hivyo tukae kwenye Ibada, tuwe watu wa neno na Maombi.
- Tunapokuwa madhabahuni mioyo yetu iwe kwa Mungu na si kwa watu. Wapiga vyombo tujifunze kumwabudu Mungu kwa vyombo vyetu. Wengi tunawapigia watu au tunapiga vyombo lakini mawazo yetu yako mbali sana.

2. WAIMBAJI BINAFSI NA VIKUNDI VYA UIMBAJI.
o Tusifanye huduma nyingi kwa siku Moja sehemu mbalimbali.
- Unahudumu Ibada ya kwanza kanisa hili ukimaliza kuimba unaondoka kabila ya NENO unaenda kanisa lingine kwenye ibada ya pili unakuta wamemaliza kuhubiri alafu wewe ndo unaimba, alafu ukimaliza jioni unamatasha mawili ya kuimba. Kwasiku hiyo wewe hujapata neno wa utulivu mbele za Mungu maaana nawaza kipande chako cha kuimba ili uondoke.
- Siyo kitu kizuri unaimba alafu unashuka nakuondoka. Siyo afya Kwako kiroho na kihuduma kufanya huduma namna hii. Tuwe na utulivu na tufuate uongozi wa Roho mtakatifu.
By Ps Safari Paul

No comments