KUTEMBEA KATIKA UWEPO WA MUNGU (Walking in the presence of God)


Siri kubwa ya mafanikio ya watakatifu wengi tunaowasoma kwenye biblia ilikuwa ni KUTEMBEA KATIKA UWEPO WA MUNGU. Watumishi wengi wa Mungu tunaowaona wamefanikiwa kiroho na ki-mwili siri yao kubwa ni kutembea katika uwepo wa Mungu.
Je, unataka Mungu asaidie hatima yako? Je, unataka kupata ushindi dhidi ya matatizo makubwa yanayokukabili?

Kama unataka mafanikio;kama unataka upenyo kwenye maisha yako ni lazima utambue NGUVU YA UWEPO WA MUNGU na UTEMBEE KATIKA UWEPO WAKE.
Hebu soma kitabu cha Kutoka 33:13-15
Kutoka 33:13-15,".....Naye akamwambia, Uso wako USIPOKWENDA PAMOJA NAMI, USITUCHUKUE KUTOKA HAPA."
Huyu alikuwa ni Musa akimsihi Mungu aende naye kwenye safari ya kuwatoa wana wa Israeli Misri na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi. Ukisoma kwa umakini kuanzia msitari wa 13 hadi 15 unaweza kuelewa kwa undani na kupata siri kubwa.
Musa hakuomba ishara na maajabu au miujiza wakati huu bali alimuomba MUNGU amwoneshe njia na sio tu kumwonesha njia bali kutembea pamoja naye.
Na Mungu alimjibu Musa kuwa UWEPO WAKE UTAENDA NAYE.
Wakristo wengi wanapuuza sana kuhusu uwepo wa Mungu.Wengi hawaoni umuhimu wa Uwepo wa Mungu.Hata watumishi wengi wa Mungu hawajui kuhusu NGUVU YA UWEPO WA MUNGU.
Kuwa na UWEPO WA MUNGU ni jambo la msingi kuliko fedha na dhahabu.Kutembea na UWEPO WA MUNGU kuna thamani kuliko UMAARUFU.
Uwepo wa Mungu ukiwa juu yako unaweza kwenda popote. Uwepo wa Mungu ukiwa juu yako hutahitaji kutafuta miujiza na ishara bali miujiza itakufuata wewe.
Ni hatari kuishi nje ya uwepo wa Mungu.Nje ya uwepo wa Mungu kuna Maradhi, umaskini, kuchukiwa, kukandamizwa, kudharauliwa, hofu, dhambi n.k
Swali la kujiuliza:Je, unatembea katika uwepo wa Mungu?Je, uwepo wa Mungu umetoweka kwenye maisha yako?
Ni vema ufanye juu chini kuhakikisha unatembea na UWEPO WA Mungu.
Hebu tusome Zaburi 51:11
• Zaburi 51:11,"Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee."
This is a powerful prayer.Ni ombi lenye nguvu. Mwandishi wa Zaburi alikuwa anasema kama kuna kitu Mungu alikuwa anataka kumnyang'anya, amnyang'anye kila kitu lakini sio UWEPO WA MUNGU. Alikuwa anamsihi MUNGU ASIMNYAMAZIE.Hata kama kuna kosa alilifanya na alitakiwa kutiwa chini ya nidhamu;Alikuwa tayari kupokea adhabu yo yote lakini si kunyamaziwa na Mungu.
Tunahitaji uwepo wa Mungu kwenye maisha yetu.Uwepo wa Mungu ni muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Musa alikuwa akipambana na wana wa Israeli. Mara nyingi walikuwa wakimwinukia na kutaka kumshambulia.Kuna wakati walitaka kumponda mawe lakini alikumbuka ahadi ya Mungu juu yake aliyosema naye kuwa,"UWEPO WANGU UTAKWENDA PAMOJA NAMI."
Hiyo ahadi iliendelea kumpa nguvu ya kusonga mbele na aliweza kuwaongoza wana wa Israeli salama.
Unapokuwa na uwepo wa Mungu;hata kama ukikutana na changamoto yoyote hauta ogopa.
Ukitembea na uwepo wa Mungu Hutatetereka.
• Leo Wakristo wengi wanajikuta wanashambuliwa sana na maadui kwa sababu hawatembei katika uwepo wa Mungu.
• Biashara nyingi zinashambuliwa kwa sababu hazina uwepo wa Mungu.
• Ndoa nyingi na familia nyingi zimeshambuliwa kwa sababu hazina uwepo wa Mungu.
• Leo maadui wamepata nguvu za kutudhuru kwa sababu ya kushindwa kutembea katika uwepo wa Mungu.
• Leo maadui wamejipenyeza kwenye maisha yetu kwa sababu ya kushindwa kutembea katika uwepo.
Ni muhimu mpendwa unayesoma huu ujumbe utie bidii katika kuutafuta uso wa Mungu na uwepo wake.(Zaburi 105:4 )

JINSI YA KUTEMBEA NA UWEPO WA MUNGU
1. Okoka kweli kweli, Acha dhambi, Acha kuhalalisha dhambi, Uwepo wa Mungu haukai kwa wenye dhambi. Dhambi inatutenga na uso wa Mungu.
2. Usicheze na muda wako wa maombi na kutafakari. (Don't play with your prayer and quiet time)
Siku ina masaa 24.Tenga muda wa maombi,kusoma neno na kutafakari ukuu na uweza wa Mungu.
Danieli alifahamu siri hii.Yeye alikuwa akiutafuta uso wa Mungu mara tatu kwa siku.
• Daniel 6:10
3. Jenga tabia ya kukusanyika na wenzako katika ibada.Maana wawili au watatu na zaidi wanapokusanyika na kumwita Mungu kwa imani.Mungu hushuka.Kuna umuhimu wa kukusanyika katika ibada.
• Waebrania 10:25
4. Uwe na shauku ya kumjua Mungu na tamani kukaa na kutembea na uwepo wa Mungu.
• Zaburi 42:1
5. Jifunze kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu. Ni Mtu na si KITU. Ni Mungu anayetenda kazi na wanadamu sasa.
6. Mwombe Mungu akuoneshe njia ya kufuata. Usifanye kitu kama hujamshirikisha Mungu. Usifanye maamuzi magumu yanayohusu hatima yako kama hujamshirikisha Mungu. Usiruhusu kuingiza mtu kwenye maisha yako kama hujamshirikisha Mungu.

No comments