Ebenezer Daniel-Tabia za Adamu (Official Music Video)


Shalom watu wa Mungu, Nawasalimu katika jina la Yesu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuweza kukuletea na kutambulisha huduma mpya/wimbo mpya kutoka kwa ndugu yetu katika kristo Yesu.  "Ebenezer Daniel." ameachia audio na video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tabia za Adamu.

Kabla yote nilipata nafasi ya kumfahamu Ebenezer kupitia moja ya marafiki zangu niliokuwa nikifanya nao kazi ambaye ni Video Director kwa jina la Wisdom; alikuja na wimbo ambao alikuwa ameufanyia video ambao ulikuwa ni wa huyu Ebenezer kwa wakati huo alikuwa akifahamika kama Dallor Day na alikuwa akiimba muziki wa Bongoflava. Hapo ndio safari ya kumfahamu huyu Ebenezer ilipoanzia. Kikubwa zaidi nilichogundua kutoka huyu ndugu ilikuwa ni ile shauku yake ya  kuhangaika huku na kule kuweza kuhakikisha kazi zake za sanaa zinafika kila mahali na anatambulika kama moja ya wasanii wanaochipukia katika tasnia ya muziki. 

Story za ndani zinadai aliwahi kuwa na mahusiano ya karibu na moja ya msanii mkubwa na mkongwe katika kiwanda cha Bongoflava (sitamtaja jina) lakini alikuwa akiwekwa benchi muda wote na asipatiwe nafasi zaidi ya kuonyesha kipaji na uwezo aliokuwa nao. Najua hayo yote huenda ilikuwa ni sababu ya Mungu kuweza kumsogeza karibu ili atumike chini ya mkono ulio hodari wa Mungu. Siku zikapita akapata nafasi nyingine tena ya kuwa chini ya management mpya ambayo pia ilikuwa ikisimamia kazi zake za sanaa kwa wakati huo akiimba Bongoflava. Kuifupisha stori hii huko nako Mungu akasimama tena akamtokea na kumkumbusha kuwa inabidi atumike chini ya kusudi la Mungu. Kwa mujibu wa maelezo yake alipata kuitikia wito huo na kuamua kuokoka kweli kweli ili maisha yake yatumike na Mungu.  Leo hii kijana ameamua kumtumikia Mungu na hii ndio kazi yake mpya ambayo ametusogezea. Unaweza kuitazama hapa. InjiliOnline tutafanya jitihada zaidi za kumtafuta Ebenezer kwa ajili ya ushuhuda wake zaidi. 

No comments