Serikali ya Kenya yamfukuza Yesu Kristo na kumrudisha kwao; Wachungaji waliomwalika washikiliwa na Polisi


Hivi karibuni kumekuwa na picha na video zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mzungu mmoja ambaye anasemekana kuwa ni Yesu Kristo, akitembea huku na kule kuhubiri injili. Picha hizo zimeweza kuibua mawazo na mijadala mbalimbali hasa kwa wakristo na wakati mwingine kuacha mswali yasiyo na majibu kamili. Hivyo InjiliOnline tukaona ni vyema tukaingia ndani zaidi na kuweza kujua ni nini kinaendelea. 

Mtu huyu ni nani, anatoka wapi na anafanya shughuli gani? huenda hili likawa ni swali ambalo umekuwa ukijiuliza kila mara uonapo picha na video zake katika kurasa mbali mbali za mitandao ya kijamii. 

Issue ilianzia hapa baada ya ujumbe (tweet) na picha moja, iliyopostiwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter na kushirikisha zaidi ya watu 8,000. Kusomeka “a pastor from South Africa invited Jesus Christ from heaven to preach in his church”.  ukimaanisha "mchungaji kutoka Afrika Kusini alimkaribisha Yesu Kristo kutoka mbinguni ili kuhubiri kanisani kwake".

Lakini baadae picha hizo ziligundulika kuwa ni za kutoka Kenya, katika mji wa Kiserian, ambao ni kama kilomita 25 (maili 15) kusini magharibi mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi.


Mtu huyo ni mhubiri na muigizaji kutoka marekani, Jina lake anaitwa Michael Job, amekuwa akihudhuria hafla kadha wa kadha za Kikristo na mikutano ya kimataifa  kama mgeni mwalikwa na msemaji mkuu.

Anaishi Orlando, Florida, ambapo ndipo pia ilipo sehemu yake ya kazi za sanaa, Michael Job huigiza kama Yesu katika jumba la sanaa la “The Holy Land Experience”. sehemu hiyo imekuwa ikielezewa kuwa ni Jumba la kumbukumbu ya Biblia.

Huku na kule wachungaji fulani kutoka Kenya wakaona hiyo ni fursa wakaamua kumualika Yesu huyo wa maigizo katika jumba la sanaa la Holy Land Experience, wakamuita kuja nchini Kenya na kuanza kutembea na mzungu huyo katika mitaa ya Kiserani na kuwashawishi waumini kuwa mzungu yule alikuwa ni Yesu Kristo, na amerudi kwa mara nyingine kama alivyoahidi kuja kuunyakua ulimwengu. 

Taarifa za ndani zinasema serikali ya Kenya imemkamata na kumrudisha mzungu huyo ambaye alikuwa akitembea hapa  na pale akijikusanyia pesa kutoka kwa wakenya ambao alikuwa akiwalaghai kwa kuwafanyia miujiza feki na kuwapa uhakika wa kupata viti juu mbinguni.  Pia wachungaji walioshiriki kumleta mzungu huyo na kutembea naye mitaani walishikiliwa na polisi kwa maelezo zaidi. 

Video zilizomwonesha Bwana Job akihubiri mapema week iliyopita katika kanisa la Pentecostal Evangelistic Fellowship of Africa (Pefa) church in Kitengela town, Kwenye video hiyo muhubiri huyo alionekana kutoa ahadi za miujiza na uponyaji, kwa hizo ambazo alipata pingamizi kali kutoka kwenye mitandao ya kijamii. 

Hii sio safari yake ya  kwanza kuja Afrika, taarifa zinadai kuwa mapema mwaka huu Yesu huyo alikuwa nchini Togo. (Huenda pia Togo walichezea janja janja ya Yesu huyu feki. 😀😀😀😀😀 )


No comments