Jehova Wanyonyi: Jamaa aliyejitokeza hadharani na kujiita yeye ni Mungu; Alikuwa na wake 70, Watoto 300 na waumini 3000


Kwa wengi Mungu hana mfano, ni mkuu wala hatagemei yeyote kwenye uamuzi wake. Wala haonekani kwa macho maangavu ila wanadamu huwasiliana naye kupitia njia ya maombi. Akiwajibu wanadamu kulingana na mapenzi yake. Lakini katika kijiji kilichoko Kaunti ya Uasin Gishu, kuna mtu ambaye alijitokeza na kujitwaza hadhi ya mungu. Mtu huyu anafahamika kwa jina la Wanyonyi

Wanyonyi anaaminika kuwa alizaliwa kati ya mwaka 1924 na 1925 katika Kaunti ya Bungoma, magharibi mwa Kenya. 

Masaa yakaisha, siku zakapita, miezi ikakatika, na miaka ikasonga mbele jamaa akaibuka na kubadili jina lake na kuanza kujiita Jehovah Wanyonyi, hiyo ilikuwa ni mwaka 1957 ambapo ndiyo wakati alianza huduma yake rasmi, na huku akijitangaza kuwa yeye ni mungu anayeishi katika kijiji cha Chemororoch, Kaunti ya Uasin Gishu, Magharibu mwa Kenya.

Katika mazungumzo yake yote Jehova Wanyonyi alidai kuwa yeye ni Mwenyezi Mungu na Yesu Kristo ni mwanae. Alitangaza pia Mlima Elgon ambao ulikuwa karibu na makazi yake ulikuwa ni Mlima Sayuni.

Madai ya Wanyonyi kuwa Mungu yalikuwa yakitumiwa kwa baadhi watu wa vijijini (local people) kuwashawishi kutoa mali zao na kumpatia Wanyonyi, Kisha Wanyonyi huzichukua na kuzigawa kwa wafuasi wake. Story za ndani zinasema jamaa aliiomba Serikali ya Kenya impatie kiasi cha Shilingi bilioni 3 za Kenya ($ 34.6 Million), Na serikali haikumpatia Wanyonyi pesa hizo, Basi unaambiwa jamaa akapata hasira akasema ataiadhibu Kenya kwa kutompa kiasi hicho cha pesa. 

Wanyonyi aliweza kujenga makazi (ngome) yake mwenyewe iliyokuwa ikizungukwa na wafuasi wake, na huku rangi nyekundu ikitawala kila pande za makazi ya Wanyonyi (Rangi nyekundu iliashiria Dunia itafikia mwisho wakati wowote)


Alidai kulikuwa na njama nyingi za kuweza kumwua lakini zote zilishindikana zikiwemo, mateso makali ya kutoka kwa wakoloni na serikali, vifungo vya jela, vyote vilishindwa kwasababu yeye ni Mungu, “Nilikuwa ni mtu wa kuogopwa jela, hakuna askari aliyethubutu kunyoosha mkono wake kwangu kama walivyokuwa wakifanya kwa wafungwa wengine. Hata simba na nyoka wakali hawakunisogelea karibu yangu, badala yake walikuwa wakikimbia mbali nami. 

Wanyonyi, kwa miaka mingi alitabiri mwisho wa dunia - ikiwa ni pamoja na 1995, 2000, na 2002. ambapo tabiri hizo zilizua taharuki katikati ya wafuasi wake. Na baadae tabiri hizo zilikuwa batili (Uongo) kiasi cha kupelekea kupoteza wafuasi wengi.

Viongozi wa Kikristo katika eneo hilo wamemshtaki kuwa ni mwendawazimu, nabii wa uongo na mambo mengine mbali mbali, lakini hakuna mtu aliyewahi kuonyesha kuwa jamaa amefanya chochote kinyume na sheria. Hivyo mamlaka hazikuweza kumzuia juu ya madai yake na kazi zake. 

Wanyonyi, alikuwa na wake 70 na watoto 300 na idadi ya wajukuu na watukuu isiyojulikana. Na inasemekana Wanyonyi alikuwa na wafuasi takribani 3000

Wanyonyi, alifariki dunia 18 July 2015. No comments