THE PROFILE: KUTANA NA KIJANA SAMUEL NWACHUKWU MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA NIGERIA ANAYEITIKISA DUNIA


All the way kutokea UK. The Profile ya InjiliOnline leo tunakuletea huyu jamaa anayejulikana kwa jina la “CalledOut Music.” Picha linaanza pale alipozaliwa mnamo tarehe 18/04/1995 na kupewa jina la “SAMUEL NWACHUKWU.” alizaliwa na kulelewa nchini Nigeria (Sasa umeelewa hilo jina Nwachukwu lilipotokea; huyu ni pure African) alipofikisha umri wa miaka 12,  yeye pamoja na wazazi wake (Familia kwa ujumla) walihamia United Kingdom “UK.”

Story za ndani zinasema Samuel  alianza kuonyesha kipaji chake cha kupenda muziki angali akiwa mdogo kabisa kwani katika umri wa miaka 7 alianza kupiga Piano kanisani na baadaye baba yake mzazi aliamua kumnunulia kinanda ambacho kilizidi kumuongezea motisha katika mapenzi ya muziki.

Muda wa CalledOut Music uligawanyika katika elimu na pia kuandika mamia ya nyimbo ambazo alikuwa akaziandika katika chumba chake cha kulala, miaka mingi katika utayarishaji wa kazi za muziki za  wasanii wengine, CalledOut Music aliamua kugeuka na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe ambapo tarehe 18/04/2016 katika siku yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa na kutimiza miaka 21 aliachia wimbo wake wa kwanza “Working On Me.”  akiwa kama solo artist. Kuanzia hapo ndiyo safari yake ya kimuziki ikaanza kuelekea worldwide.

Akiwa kama mkristo aliyejitoa kikamilifu, Muziki wa Samuel una utofauti wa kipekee sana kwani huonyesha sana Imani yake kwa Yesu, Jinsi anavyoweza kushughulikia masuala ya watu kupitia uimbaji wa Injili na watu wakampokea Yesu. Samuel ameweza kuteka muitikio wa watu wengi hasa kizazi hiki kipya cha Gospel na kumpelekea kuchota pongeza nyingi kutoka kila kona ya Dunia kwa huduma yake. Amekuwa akipongezwa na waimbaji wengine wakubwa wa Muziki wa Injili Duniani kama  Fred Hammond & Richard Smallwood lakini CalledOut Music anasema kuwa; amekuwa akimuangalia Kirk Franklin kama mtu wa mfano kwake.

Alianzisha huduma ya Injili inayoitwa “Called Out.” yenye lengo la kumfahamisha kila mmoja kuwa na Imani na fikra ya kwamba sote tumeitwa kwa ajili ya huduma ya Mungu.
Huduma ya muziki wa Samuel imeweza kufungua mafanikio makubwa toka alipoanza kufanya kazi kama solo artist huku kwa sasa akitamba na kazi yake mpya inayofanya vizuri “Awesome Wonder.” Iliyotoka Jun 15, 2019.

Hizi hapa ni baadhi ya kazi kutoka kwa CalledOut Music


Cc:  @calledoutmusic
Written By: @tabasamu_tz

No comments