MFAHAMU KWA UNDANI ZAIDI PHIL THOMPSON KUPITIA THE PROFILE YA INJILI ONLINEPhil Thompson ni mtunzi na muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Boston, Massachusetts, kabla ya kuanza kupata mafanikio ya kazi zake akiwa kama msanii huru yaani  “Solo Artist.” @philthompsonworship aliwahi kuwa mwanachama wa kikundi maarufu cha muziki wa injili kilichojulikana kama “ASHMONT HILL.”  (Ashmont Hill; iliundwa na akina, Deborah Bullock, Wil Bullock, April Joy Mtyora & Phil Thompson)


Mwaka 2018 @philthompsonworship alitoa albamu yake ya kwanza kama Solo Artist, ilyokwenda kwa jina la “MY WORSHIP.” yenye mjumuisho wa nyimbo 11 kali zenye mguso wa pekee.
Story zinasema kuwa @philthompsonworship alikuwa akiimba tangu utoto, lakini hakuwahi kuandika nyimbo zake mwenyewe hadi pale alipofikisha umri wa miaka 30…… (Usishangae jamaa anaonekana kama mkubwa hivi halafu ana albamu moja hadi sasa) 😀😀 jokes ……..


Mbali na kuwa muimbaji anayejitegemea, Jamaa pia ni worship leader wa kanisa la Jubilee Christian Church.  Pia ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuandaa kazi za muimbaji mwingine nguli wa muziki wa injili kutoka marekani “JJ Hairston.” (huyu profile yake itakujia hivi karibuni) mchango wake pia hauwezi kusahaulika ndani ya Jubilee Worship na Ashmont Hill.

Albamu yake iliweza kushika namba za juu kwenye chart mbali mbali ikiwepo Billboard na kushika namba 1. Album hiyo iliandaliwa na kutolewa chini ya studio za JJ Hairston’s Jamestown Records.

Wengi wetu (hasa wabongo 😀) tumemfahamu huyu jamaa kupitia wimbo wa “Atmosphere Shift.” aliouimba pamoja na Jubilee Worship.
Mbali na hayo kazi zake nyingine zilizoweza kumtambulisha vizuri kama solo artist ni pamoja na
1 Chasing Your Glory
2 My Worship (Live Extended)
3 The Ultimate (feat. Shana Wilson)
4 Home Away from Home
5 You Love Good

Kutana zaidi na kazi za Phil ThompsonCc: @philthompsonworship
Witten By: @tabasamu_tz

No comments