Video: Mchungaji, Angel Obinim Alala na Mwanamke Katika Kanisa Lake Ili kumpa Muujiza wa Kupata Mume Wake


Leo katika pitapita zetu kwenye mitandao ya kijamii Injili Online tumeweza kunasa video inayomuonyesha Mchungaji Angel Obinim kutoka Ghana akilala na mwanamke katika Kanisa lake,  ikiwa kama njia ya kufanya muujiza kwa mwanamke huyo ili apate mume.

Mbele ya waumini wake, Mchungaji Angel Obinim alimwambia mwanamke huyo kulala juu ya sofa wakati pia alijiunga naye na kulala pamoja huku akimshikilia (kumbatia) kwa nguvu. Katika mchakato huo, mwanamke huyo alianza kuubusu mkono wa mchungaji wake. Na wakati huo kusanyiko la kanisa hilo lilipiga kelele za shangwe na nderemo kuunga tukio hilo.

Kwa mujibu wa mchungaji Angel Obinim hivyo ndivyo mwanamke huyo atakavyolala na mume wake wakati muujiza wake utakapo kamilika.
Naam, kabla ya kufikiria kumtukana Obinim kuhusu video ya utata au kutoa maoni kinyume naye juu ya video hiyo, soma kile alichosema wiki chache zilizopita.

“The more you insult me, the more I love you. Even if you write any bad comment about me I still love you and will reveal myself to you in your dreams either this afternoon or in the night” "

“Go ahead and insult me on Twitter, Facebook and Instagram more than anyone else, what I can assure you is that I certainly appear in your dreams and there is no doubt about that”

“If you hear that anyone is insulting me in Ghana, tell the person Angel Obinim loves him and that he will appear in his dreams”.No comments