AKOTHEE KUACHA MUZIKI WA KIDUNIA, AWEKA WAZI MPANGO WA KUFANYA MUZIKI WA INJILI


Sio tu kuokoka, Akothee ana mpango wa kuacha kabisa muziki wa kidunia na kuanza kufanya muziki wa Injili.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Akothee alikaririwa akisema:

"Tumesahau kuwasifia na kuwapongeza wasanii wetu na tunawakumbatia wa nje. Utakuta wimbo ni mbovu kabisa lakini unakuwa Hit hapa Kenya." alisema Akothee na kuongeza kuwa

"Ninawapongeza wasanii wote wa injili kwa sababu kanisani hakuna yoyote ambaye anahitaji kukuonesha ushirikiano. Hauihitaji kujipongeza mwenyewe kwasababu kanisa kila siku limejaa. Ndio maana nataka kuhamia huko (gospel) kwa sababu ni rahisi kwangu. Kila mtu anamuhitaji Yesu, au sio?"

No comments