Wasanii wakubwa wa Gospel nchini Kenya, wakiri kumuingilia kimwili mwanamke ‘Threesome’ na kumuambukiza gonjwa la zinaa.


Wasanii wakubwa wa muziki wa Injili nchini Kenya, DK Kwenye Beat na Hope Kid wamejikuta katika kipindi kigumu nchini humo baada ya kukiri kumuingilia kimwili mwanamke aliyelalamika kwenye vyombo vya habari kuwa ameambukizwa gonjwa la zinaa (STI).

DK kwenye Beat yeye ndiye aliyeanza kukiri kushiriki tukio hilo, ambapo amejirekodi video ya dakika 5, huku akihojiwa na muimbaji mwingine wa Gospel, Size 8.

DK Kwenye Beat amemuomba msamaha mchumba wake, Sherry Shanice na mashabiki wake kwa kitendo hicho.
Imeelezwa kuwa msichana huyo anatoka Mjini Nakuru, na alianza mawasiliano kwa njia ya mtandao na masanii Hope Kid.

Msichana huyo (20) ambaye ameambukizwa gonjwa la ngono, amesema alitongozwa na Hope Kid na kisha baadae kumtumia nauli ya kwenda Nairobi kuonana.
Anasema alipofika Nairobi mwezi Novemba mwaka jana , Hope Kid alimpeleka nyumbani kwa DK Kwenye Beat ambapo walimfanyia unyama huo kwa wiki moja.
Katika maelezo ya msichana huyo, amedai kuwa baada ya kufanyiwa kitendo hicho mwezi mmoja baadae DK kwenye Beat alimfuata tena Binti huyo huko Nakuru ambapo anadai alifanya naye mapenzi bila jambo lililopelekea kuambukizwa gonjwa hilo la zinaa Human Papilloma Virus (HPV) .
Kwa upande mwingine, Hope Kid naye amewaomba radhi mashabiki wake na kudai kuwa alianguka kiimani.
Hata hivyo, licha ya kuomba msamaha Wakenya wengi wameendelea kuwaandama wasanii hao kwa kutaka wachukuliwe hatua za kisheria. Tazama video

No comments