MWALIKO WA KUHUDHURIA JUKWAA LA UCHUMI WA UFALME WA MUNGU (2019 KINGDOM ECONOMIC SUMMIT)


Kwa kipindi kirefu Kanisa la Tanzania limepita katika kipindi kigumu cha kifedha kwa waumini, huduma, watumishi
wenyewe binafsi na makanisa wanayoyaongoza na hata familia zao. Hii imesababisha Wakristo kupata ugumu katika
maisha yao na huduma walizoitiwa na hata kupelekea wakati mwingine kukata tamaa. Kanisa limejikuta katika hali ya
kupoteza mvuto kiuchumi, heshima, umuhimu wake katika jamii na taifa kwa ujumla, hivyo kushindwa kuwa mfano wa
uweza na utajiri wa Kiungu katika Kristo Yesu.

Ili tuweze kukabili vizuri changamoto hiyo, umeandaliwa mkutano wa kitaifa, Jukwaa la Kiuchumi wa Ufalme wa Mungu
(Kingdom Economic Summit), utakaojumuisha madhehebu yote ya Kikristo katika ukumbi wa Mlimani City Conference
Centre Dar es Salaam, kwa siku tatu kuanzia tarehe 05 Machi 2019 mpaka 07 Machi 2019 saa saba mchana mpaka saa
mbili usiku. Mada kuu ni “Kutimiza Mamlaka yako ya umiliki/utawala (Fulfilling Your Dominion Mandate)” na lengo la
mkutano huu ni kumsaidia mkristo mmoja mmoja na kiongozi wa kanisa kuweza kukabiliana na Changamoto za kiuchumi
na pia kuliandaa Kanisa la Tanzania kuinuka na kuchukua nafasi yake katika nchi.

 Majira ya Mungu kwa Tanzania kuamua
juu ya hatma yake na kuathiri Afrika nzima umewadia; na nafasi ya kiungu kwa Kanisa la Tanzania kutawala majira yajayo
ni sasa. Mkutano umeandaa wanenaji ambao wana ushuhuda wa kinadharia na vitendo katika maisha yao ya kiuongozi,
kihuduma na kiuchumi. Wameona Mungu akiwainua kutoka katika hali za chini sana hadi kuwa watu mashuhuri duniani
waliofanikiwa sana na kuheshimika duniani kote. Baadhi ya wanenaji hawa ni:

i) Dr. Bill Winstom (USA): Ni kiongozi, mfanyabiashara aliyefanikiwa sana pia ni mhubiri mkubwa wa kimataifa na
aliyefanikiwa sana kihuduma, kiuongozi na kiuchumi. Ni mchungaji anayeongoza kanisa kubwa la waumini zaidi ya elfu
ishirini Marekani linalomiliki biashara kubwa mbalimbali Duniani kama maduka makubwa (shopping malls) na vyuo vya
kufundisha wafanyabiashara walio okoka jinsi ya kufanikiwa kibiashara na kutajirika kwa kutumia kanuni za kibiblia.

ii) Dr. Nigel Chanakira (Zimbabwe): Kiongozi mkubwa kibiashara aliyeokoka na aliyebobea sana kwenye masuala ya
kiuchumi, kifedha, utawala bora na maadili. Aliwahi kuwa Mmiliki wa Bank kubwa ya Kingdom Bank lakini pia ni
mwenyekiti wa Taifa wa uwekezaji nchini Zimabwe. Ni Raisi wa taasisi ya Success Motivation Institute Africa. Pia ni
mshauri kwenye taasisi nyingi za kimataifa pia ni mshauri wa viongozi wakuu mbalimbali duniani.

iii) Wanenaji wengine ni Dr. Abu Bako (Ghana), Dr. Joe Mzuanda (Tanzania),Kelebogile Moloko(SA),Prof.Judiffier
Pearson(Marekani), Jason Benedict (Marekani), pamoja na viongozi wengine wa kanisa, Serikali na biashara hapa Tanzania.
Walengwa katika mkutano huu ni viongozi wa Kanisa na waumini wote, wafanyabiashara, wanasiasa, viongozi mbalimbali
wa Umma na sekta binafsi. Mkutano umeandaliwa kwa ushirikiano wa Kamati ya Umoja wa Makanisa-Dar es Salaam
Tanzania,Taasisi ya Bill Winston Ministries ya Marekani inayoongozwa na Dr. Bill Winston pamoja na Kingdom
Leadership Network Tanzania (KLNT).

Pia kwa kushirikiana na Taasisi na huduma nyingine mbalimbali za ndani na nje ya
nchi. Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa tunakualika rasmi kushiriki katika mkutano huu muhimu sana kwa nchi yetu
na kutusaidia kuusoma mwaliko huu kwawaumini ibadani tarehe 17 Machi, 2019, 24 Machi pamoja na 03 March, 2019.
Kwa kutambua umuhimu wa mkutano huu, KLNT inapenda kukukaribisha katika mkutano huu na imetoa sadaka ya
ushiriki bila malipo kuanzia saa kumi jioni mpaka saa mbili usiku ila kujiandikisha kupitia www.kingdomleadership.ne.tz ni
lazima kabla ya mkutano.

Warsha na mafunzo itakuwa na gharama za kushiriki 150,000Tsh kuanzia tarehe 01 March,
2019. Ukilipia mpaka tarehe 28 Februari ni 130,000Tsh. Tumeambatanisha ratiba nzima ya mkutano pamoja na fomu za
kujaza kuthibitisha ushiriki wako.

Kwa mawasiliano zaidi piga 0764 001 245 au info@kingdomleadership.ne.tz
Wako katika utumishi,
Hon. Ibrahim. M. Kaduma Isaac Mpatwa
Bodi ya Wadhamini KLNT Mkurugenzi Mtendaji KLNT

No comments