Mchungaji kutoka Zimbabwe akamatwa kwa kuuza tiketi za kwenda mbinguni kwa $500


Imeripotiwa kuwa watu wawili ambao ni viongozi wa kanisa huko Zimbabwe, Mchungaji Tito Watts na mkewe, Amanda Watts, wamekamatwa na jeshi la polisi nchini humo kwa kuuza tiketi za kwenda mbinguni kwa waumini wa kanisa lao.

Kwa mujibu wa matandao wa  Egypt Today, polisi wamedai kuwa mchungaji huyo pamoja na mkewe waliwalaghai watu kadhaa kununua tiketi ambazo zingewapa mpenyo wa kwenda mbinguni moja kwa moja na kila teketi iligharimu takribani Dollar 500  ambazo ni sawa na millioni 1.2 kwa fedha ya kitanzania.


Chanzo cha habari kiliongeza kuwa, tiketi hizo zilikuwa zina kibali cha kuingia mbinguni bila kupitia sehemu ya hukumu

Mchungaji Watts aliwaambia watu ambao waliokwenda kutafuta wokovu kanisani kwake kuwa tiketi hizo zilitengenezwa kwa dhahabu ngumu na kila tiketi moja ilikuwa inahifadhi nafasi ya mtu juu mbinguni

Aliongeza pia kwa kusema ni Yesu ndiye alimpatia tiketi hizo alipokuwa nyuma ya mgahawa wa KFC na kumpa maagizo akaziuze ili apate pesa ya kutoka nje.

"Nilikutana na mgeni aitwaye Stevie ambaye alisema kama ningepata pesa angeweza kunichukua mimi na mke wangu juu ya roketi yake na kuruka hadi kwenye sayari nyingine ambayo imetengenezwa kwa Cocaine. Mke wa mchungaji huyo alisema kuwa yeye na mumewe walitaka kuondoka sayari hii (Dunia) hadi sayari nyingine kama walivyoahidiwa na Stevie ili waweze kuvuta moshi wa cocaine". Alisema Watts.Ndani ya kisa hicho pia iliripotiwa kuwa polisi walimkamata na zaidi ya Dollar $10,000 cash. Hiyo sio mara ya kwanza kwa mchungaji huyo kukabiliwa mashitaka kama hayo. Mwaka 2015 yeye pamoja na mkewe waliwahi kuhusishwa katika kesi ya ulaghai kama huo.

Moja ya wateja walionunua teketi kwa wanandoa hao aligundua kuwa amechezewa mchezo mchafu baada ya kuuziwa tiketi ya mbao ambayo ilipakwa rangi ya dhahabu.

"Ninahitaji $500 yangu kwanini waniuzie kapande cha mbao kilichopakwa rangi, Tito na Amanda wanastahili adhabu ya kifo kwa yale wanaoyafanya. wanastahili adhabu hiyo". Alisikika mmoja wa wateja waliouziwa tiketi hizo, Del Woodcock.


No comments