Wang Xiu Ying: Muhubiri kutoka China, aliyekufa kisha kufufuka baada ya masaa 17 Amesema aliona waafrika wengi wakikusanya kuni Kuzimu


Muhubiri mmoja kutoka China ambaye alifariki siku ya ijumaa iliyopita tarehe 7/12/2018 majira ya saa tatu na dakika moja asubuhi na baadae kufufuka baada ya masaa 17. Ameelezea namna ambayo alipata nafasi kutembelea Mbinguni (Paradiso) na Jehanamu (Kuzimu). Mchungaji Wang Xiu Ying alisema safari yake ya juu mbinguni aliingiliwa kati na malaika aliyeitwa Luj ambaye alimwambia kuwa wakati wake wa kufa bado haujafika. Malaika Luj akaamua kumtembeza kwa ziara fupi mchungaji huyo kuweza kumwonyesha maeneo mbalimbali yaliyopo Mbunguni, Na ziara yao ikaishia katika eneo la Shimo liwakalo moto (Jehanamu) ambapo anasema aliona waafrika wengi wakikusanya kuni katika eneo hilo. 

Malaika Luj akamwambia kuwa waafrika wengi hukusanya kuni katika malango ya kuingia Jehanamu. Hiyo inaonyesha na kuashiria kuwa bara la Afrika ni bara lililojaa dhambi na wakati wowote linaweza kukabiliana na gadhabu ya Mungu. Hivyo kwa wakati ule safari ya mchungaji Wang ikafikia mwisho na akaandaliwa kitu chenye mfano wa bomba kuweza kumrudisha Duniani kwa mara nyingine.

Muhubiri Wang Xiu Ying ambaye tayari amekwisha weka mpango kwa kutembelea nchi ya Nigeria mwezi wa kwanza amesema kuwa Mungu amemtuma kuwaonya wachungaji wanaowapotosha watu wa Mungu kuelekea katika njia ya uharibifu. Kwa manabii, makuhani, wachungaji, maaskofu, waalimu na wainjilisti ambao kwa mfano wao au mafundisho yao houngoza kondoo katika tabia ya dhambi na imani za uharibifu.


No comments