Rose Muhando abadilisha jina lake, Sasa kujulikana kama Simba wa Kike (Lioness)


Rose Muhando amebadilisha jina lake hivi karibuni baada ya video iliyosambaa mtandaoni iliyokuwa ikimuonyesha wakati akifanyiwa maombi maalumu nchini Kenya na Mchungaji James Ng’ang’a wa kanisa la Neno Evangelism Centre’s, kwa ajili ya kuondoa mapepo ambayo inasemekana yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Jumatano iliyopita wakati akifanya tamasha pamoja na mwimbaji wa Kamba, Stephen Kasolo, ambaye aliuambia umati: "Rose Muhando amebadilisha jina lake na kuwa Simba wa Kike (Lioness)."
Atakuwa akijulikana kama Simba wa Kike (Lioness) kuanzia siku hiyo.

Rose alielezea kwa nini ameamua kubadili jina lake. Alisema "Nimepitia mambo mengi sana. Matatizo niliyopitia yamenipa nafasi ya kujenga uvumilivu na ustahimilivu maishani mwangu, kwa hiyo sababu unaweza kuniita simba wa kike"

Pia aliongeza kwa kusema: "Kazi yangu ni kuwinda. Mimi siogopi kitu chochote. Ninapopiga kelele, jehanamu inajua kwamba nimepiga kelele na jehanamu nzima ina inatetereka. Sitaweza kunyamaza na kukaa kimya mpaka Mungu atakapo pokea utukufu wote. "

Rose na Stephen Kasolo wana wimbo wa  pamoja uitwaye Hautasumbuka Tena.  Rose alisema Stephen Kasolo amekuwa naye bega kwa bega na hata kumkutanisha na watu wenye ushawishi ambao wamemsaidia".

Pia amemshtaki meneja wake aitwaye Nathan, kuwa nyuma ya mateso yake yote.

No comments