Roho ya Urafiki (The spirit of friendship)


Shalom watu wa Mungu.

Leo nataka nizungumze na wewe jambo hapa kuhusu roho ya urafiki. Mara nyingi watu tunautazama urafiki kwa jinsi ya mwili bila kutambua kuwa urafiki unajengwa rohoni na sio mwilini, ndiyo maana utamsikia mtu anasema "Jamani mimi fulani roho yangu imemkataa". Maana yake ni nini, roho haikuona jambo ambalo linaweza likawaunganisha hawa watu wawili. Sasa najua una marafiki wengi tu mpaka wengine unawaita "best friends". Umeshawahi kujiuliza ni jambo gani linawaunganisha?

Nikitaka kukujua wewe sina haja ya kukuchunguza, nitamtazama rafiki yako tabia zake, maana kuna jambo linalowaunganisha ambalo kila mmoja wenu analo. Petro alimkana Yesu mara ya kwanza akasema simtambui mtu huyu, jamaa wakagoma wakasema ata ongea yako inaonesha wewe ni mmoja wao, akaenda sehemu nyingine, jamaa wakasema hakika huyu naye ni mmoja wao, akasema sijui msemalo, wakakataa wakamwabia ata tembea yako inaonesha wewe ni mmoja wao. Ongea na tembea ya Petro vilitosha kumdhibitisha kuwa ni mwanafunzi wa Yesu. Je hivi vitu vilitoka wapi? Kwenye maisha aliyoishi na Yesu pamoja na urafiki wao, mitume waliishi na Yesu mpaka wakafanana na Yesu. Yesu mwenyewe alisema "Mkiniona mimi mmemuona Baba", alikuwa anatuambia yeye na Mungu Baba hawana utofauti ata kidogo. 


Sasa na wewe nikitaka kukujua sia haja ya kukuchunguza nitatazama mienendo na tabia za rafiki yako, maana alivyo mtu ndivyo alivyo rafiki yake, kuna roho inawaunganisha. Sasa nataka nikuulize wewe, unajua ni roho ipi inakuunganisha wewe na rafiki zako? Kuna wengine ni marafiki kwa sababu ya masomo, wengine ni marafiki kwa sababu wanaabudu Imani moja, wengine ni marafiki kwa sababu ya kazi, wengine marafiki kwa sababu wanaishi nyumba moja, wengine urafiki wao ni kwa sababu ya umbea, wengine marafiki kwa sababu ya wizi, wengine marafiki kwa sababu ya utapeli, wengine marafiki kwa sababu ya vyama, nk.

Sina tatizo na jambo/roho inayowaunganisha, swali langu ni je hilo jambo linalowaunganisha linampa Mungu utukufu? Je linakujenga ama unapoteza muda wako bila kujua? Lina faida kwako na kwa ufalme wa mbinguni au hasara tu? 
Tafakari. 


Cc 
Mwalimu Ansbert Justus:

No comments