UJUMBE KUTOKA KWA PASTOR SAFARI PAUL 'CONNECT WITH GOD'


Watu huamini kwamba ili ufanikinikiwe katika mambo yako, mfano upate kazi, biashara, au mafanikio yoyote unahitaji CONNECTION na watu sahihi. Wanasema uwe na network nzuri, kutana watu wenye majina au wenye nafasi zao. Wanasema lazima ufahamiane na mtu flani ili utoboze.
Wengi wamekata tamaa ya kufanya mambo kwasababu hawana watu sahihi wakuwapa connection ili wafanikiwe.

MIMI naseman unachohitaji ni GOOD CONNECTION NA MUNGU JEHOVAH. Akiamua kutenda hakuna atakaezuia kusudi la Mungu katika maisha yako. Uwepo wa Mungu katika maisha yako huleta Kibali na Kibali cha Mungu kitafungua milango mbele yako. 
Daudi hakuwa na Connection na Nabii Samuel lakini alikuwa na connection na Mungu na Mungu akafanya connection Daudi akapakwa mafuta kuwa mfalme.

YUSUFU alikuwa mfungwa hakuwa na Connection na Farao japo alikuwa na kipawa na upako. Lakini Mungu alitengeneza connection mpaka akawa waziri mkuu wa Misri.

Yahana 15:7. Inasema ukikaa ndani Yesu na maneno yake yakaa ndani yako, Omba jambo lolote na Bwana atafanya.

Mwamini Yesu na uwe na mahusiano nae. Ishi sawa na neno la Mungu na uwe na ushirika nae. Amini kwamba atakubariki na atakuinua.

YOU ARE BLESSED usiogope, usikate tamaa weka imani yako kwa Mungu. Yesu hatakuacha kamwe maana anakupenda. 
Umebarikiwa.

Ps Safari Paul

No comments