The Profile: Mfahamu Zaidi Mercy Masika Muguro Muimbaji wa Nyimbo za Injili Kutoka Kenya


Mercy Masika ni mtunzi, mwandishi na mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya. Alifahamika kwa mara ya kwanza mwaka 2003 kupitia wimbo maarufu “Amukomete” (Amka), uliomfungulia safari yake ya muziki.

Alianza safari ya muziki 1994; na anasema ulikuwa wito wa Mungu kumuimbia. “Uimbaji wangu ni wito kuhubiri neno la Mungu kupitia nyimbo,” anasema Mercy Masika.

Hata hivyo, anasema ufanisi wake katika fani ya muziki umefanikishwa na mama yake mzazi Bi Agnes Masika ambaye alikuwa mmoja wa waimbaji wakuu wa kwaya ya kipindi cha runinga ya KBC ‘Sing and Shine’, iliyovutia wengi miaka ya zamani. “Nimefuata nyayo za mama ambaye amenikuza kimuziki"

Anasema kupitia juhudi za mama yake, yeye pamoja na ndugu zake waliweza kuhusishwa kwa kipindi cha ‘Joy Bringers’ ambapo walikuwa miongoni mwa waliotumbuiza. “Nilishawishika kuzindua albamu yangu ya kwanza ‘Nobody Like Jesus’ nikiwa darasa la sita, wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 12,” Anaongeza kuwa albamu hiyo alimshirikisha mama yake.

Alipojiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machakos, msanii huyo aliendelea kupalilia kipaji chake cha kuimba

Katika shule ya upili alizindua albamu yake ya pili ‘Roses Will Bloom Again’, ambapo Paul Kigame ndiye alimsaidia sehemu kubwa kuifanikisha. Anaongeza kuwa aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa kwaya za shule hiyo.

Na wakati alipojiunga na Chuo Kikuu cha Daystar mwaka 2002, Hapo ndipo alikua kwa kiasi kikubwa kimuziki.

Alizindua albamu yake ya tatu ‘Wendo Waku’ (Mapenzi yako Mwenyezi Mungu) inayojumuisha nyimbo za Kikamba na Kiswahili kama ‘Nisamehe’, ‘Amokemete’. Anasema kwamba albamu hiyo ilimzolea sifa chungu nzima na kumfahamisha nchini na kiwango cha kimataifa.

Tangu 1994, Mercy amezindua zaidi ya albamu sita.

Nyimbo kama Nikupendeze, Milele, Nisamehe, This Life, Umeinuliwa, Yeye Ni Mungu, Nakupa Yote, Mtakatifu na Emmanuel pia ndizo zimempandisha hadhi mwanamuziki huyo.

Mercy amepata tuzo mbalimbali kama; 2013-2014 – PARTNER manager and ambassador for CIM 2013-2014, Groove awards –Artist of the year & Female artist of the year 2008, Mwafaka awards, miongonu mwa tuzo zingine.

Staa huyo ni mke wa David Tim Muguro. Na ni mama wa watoto wawili. 

No comments