PUNDA NI MFANO WA MIMI NA WEWE


Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;
(Yakobo 1:2)

Mkulima mmoja alikuwa na Punda ...Punda aliyedumu nae kwa miaka mingi sana aliyemsaidia shughuli za kilimo na uchukuzi... alikaa naye toka akiwa mtoto mpaka punda akawa mzee kabisa.*
🐴 Siku moja wakiwa wanatoka shambani, kwa bahati mbaya yule punda alitumbukia kwenye kisima kirefu sana ambacho kwa wakati ule kilikuwa kimekauka.
🐴 Yule Mkulima akawaza sana atafanyaje kumtoa yule punda..na baada ya kutafakari sana akasema kwanza hata hivyo huyu punda ameshazeeka ni hasara kuingia gharama za kumtoa...akaona vema tu amzike humo humo.
🐴 Akaenda kuita majirani ,wakaja na sepetu wakaanza kumwagia udongo ,mchaka na kokoto shimoni kumfukia.
🐴 Mwanzoni tu ni kama punda alijua kinachoendelea..akapaza sauti na kulia kwa sauti kali ajabu..sauti ya malalamiko...hawakujali waliendelea kufukia..kwa kutupia kila aina ya taka taka.
🐴 Baadae kidogo kwa mshangao wa wengi ghafla punda alinyamaza kimya kabisa sauti ikapotea....baada ya kutupia taka kadhaa..mkulima yule akaamua kuchungulia shimoni....
🐴 Alisitushwa mno na alichokiona.
Kila taka na mchanga ulipokuwa ukiangukia mgongoni mwa punda...alikuwa akifanya kitu cha kushangaza.
🐴 Kila udongo ulipomwangukia...alijitingisha ukamwagika na akaukanyaga akainuka juu kidogo...kila ulipokuja aliendelea kufanya hivyo hivyo...
🐴 Hatimaye baada ya Muda mkulima na majirani walishangaa kuona amefika juu kabisa ya ukingo wa kisima na akatoka kwa furaha kabisaa.
*Kuna wakati maisha yanakurushia matakataka ya kila aina, acha kulia na kupiga kelele, jitingishe...yafanye ngazi.
*Kila jaribu linalotupata ni ngazi ya kupandia.
🐴 Kamwe hatuwezi toka kwenye visima virefu kwa kulia peke yake... bali kwa kupambana kuchomoka.
🐴 Wacha waone uko kimya baada ya makombora waliokurushia...yote yapange..yafanye ngazi ya kupandia...
_*Changamoto yeyote unayopitia sasa...ni shimo na michanga..
🐴 Sisi ni zaidi ya punda. Acha kulia, jikung`ute, yakanyage ,nyanyuka juu, toka! Kanyaga Twende!.

No comments