Mfahamu kwa undani zaidi Deborah Lukalu (DL) kupitia The Profile ya Injili Online


Deborah Lukalu alizaliwa katika moja mji mkubwa na mzuri kutoka Demokrasia ya Watu wa Kongo unaoitwa Lubumbashi. Akiwa ndiye mtoto mdogo na wa mwisho katika familia yenye watoto wanne, Deborah Lukalu kwa mara ya kwanza aliuona mwanga wa Dunia tarehe 24 March mwaka fulani 🤗. Akizungukwa na kulindwa na upendo kutoka kwa kaka zake watatu ( Israel, Randy, Youri). Baada ya kifo cha baba yake. Marehemu Luc Lukalu. Mama yake Deborah, Chantal Lukalu Zahabu pamoja na watoto wake walihama Kongo na kuhamia nchini Afrika ya Kusini mnamo mwaka 2004.

Muziki umekua ni moja ya sehemu ya maisha ya Debora. Kwani katika umri wa miaka 6 Debora alianza kuonyesha kipaji chake cha kuimba. Kipaji cha Debora kiligundulika kwenye kanisa la JESUS Le Rock mjini Lubumbashi ambapo alikuwa akifanya vizuri zaidi katika kwaya ya watoto wa kanisa hilo. Kwa wakati huo alionekana kama mtoto wa ajabu na mwenye baraka kutoka kwa Mungu kwani alikuwa na uwezo wa kuandika nyimbo zake mwenyewe na kuziimba kwa umaridadi mkuu. 
Baada ya kifo cha Baba yake na baadae kuhamia Afrika ya Kusini, Moto wa Debora wa kuimba haukuweza kuzimika. Alianza kuhudhuria Ibada katika moja ya kanisa lililoitwa Faith and Victory. Ambalo lilikuwa chini ya mchungaji Mike Lwambwa ambaye baadae alikuwa baba yake wa kiroho. Debora aliendelea kukua kanisani hapo na akafanikiwa kujiunga na Kikundi cha kusifu na kuabudu ili kuweza kutimiza haja yake ya kumuabudu Mungu katika roho na kweli.

Debora alihudhuria masomo katika shule ya EastGate Primary ambapo alichaguliwa kuwania tuzo za Idols Primary zilizowakusanya watoto wenye vipaji vya kuimba kutoka afrika ya kusini, Debora alifanikiwa kushinda tuzo hiyo akiwa mshindi wa kwanza. 
Mwaka 2011 DL alipokuwa High School alifanikiwa kufungua Band yake ambayo baadae ilikuwa maarufu na kufanikiwa kunyakua tuzo 3 na vyeti vya heshima kwa kazi walizokuwa wakifanya.
Mwaka 2014 ulikuwa ni mwaka ambao DL alifanikiwa kuachia Album yake ya Law Breaker. Album hiyo Iliyotoka Rasmi tarehe 25 April 2015 kwenye tamasha lake la kwanza ambalo lilijumuisha mkusanyiko wa nyimbo za kisasa za Injili ambazo zilikuwa zikigusa mioyo ya watu kuelekea kumuabudu Mungu.

Mwishoni wa mwaka 2015 DL alichaguliwa na kushinda tuzo ya 'Best Female Vocalist'. Katika jiji la Johannesburg chini ya Voice Of Congo na IML. Deborah ambaye kwasasa ni balozi wa kanisa lake na makanisa mengi ulimwenguni na pia ni mfanyakazi katika kutuo cha Television cha Gospel For Life TV.

DL amesharikishwa na kushirikiana katika kazi za injili na wasanii wengine wakubwa wenye majina kutoka Kongo na Afrika Kusini. Kama The Dube Brothers Proghete Keke, Moise Mbiye, Michael Bakenda, Sandra Mbuyi, Dena Mwana, Herve Nzambe, Rachel Olangi, Billy Sabu Prince Yav, Apostle Narciss Majila. Hao ni baadhi tu kwa kuwataja majina yao.

DL amkuwa na mipango mingi na mikubwa ambayo ikiwemo kufungua vituo vya kulelea watoto yatima na wasiojiweza kadharika shule ya muziki ambayo itakuza na kuendeleza vipaji vyao. Na sio hapo tu bali kuinua wanawake kwa wanaume ambao wataziliwa kupitia muziki wa Injili. 

▶ Zifuatazo ni nyimbo kutoka kwa DL ambazo zilifanya vizuri kwenye soko la kimataifa la Muziki wa Injili.

➡ We Testify
➡ You Deserve
➡ Awesome God
➡ Ba Kombo Ebele 
➡ Everybody Follow Jesus
➡ Bless Me Papa
➡ Law Breaker
➡En Tu Presencia

No comments