MCHUNGAJI AKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUSHINDWA KUMFUFUA MTOTO WA MIEZI 5.


Polisi kutoka wilaya ya Luweero, nchini Uganda. Wamemkamata mchungaji mwanamke na wasaidizi wake kwa tuhuma za mauaji baada kushindwa kumfufua mtoto wa miezi 5. Mchungaji Viola Nassanga na wasaidizi wake ambao ni Juliet Nakayenga, Edith Nabuule na mwenye nyumba ambaye amelipangisha kanisa hilo Lazaro Walakira walikamatwa ijumaa iliyopita kwa kile kilichosemwa kushindwa kurejesha uhai wa mtoto Anita Kwagala.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi wa wilaya hiyo Benson Byaruhanga Mworozi. Amesema kuwa wiki iliyopita Mchungaji Viola alimwambia Asineyi Biira ambaye ni mama wa mtoto kumpeleka kanisani mtoto kwa ajili ya maombi zaidi baada ya mama huyo kwenda kwa mchungaji Viola na kueleza kuwa mtoto wake alikuwa akiumwa. Taarifa zinasema kwamba baada ya hapo mtoto hakuonekana tena hadi siku ya alhamisi ambapo kulitaarifiwa kuwa mtoto alifariki katika chumba alichokuwa akifanyiwa maombi. 
Siku ya Alhamisi Oktoba 4, Mama wa mtoto alipokea taarifa mbaya kuhusu mwanae kuwa amefariki. Lakini mchungaji Viola alimuhakikishia Biira kuwa ana nguvu na uwezo wa kuponya na kufufua wafu.

Majirani wa kanisa hilo walitoa taarifa polisi baada ya kuona harufu isiyo ya kawaida kutoka katika nyumba ambapo Mchungaji Viola na wasaidizi wake walipokuwa wakifanya maombi. "Hili ni tukio la bahati mbaya ambalo polisi wako ktk uchunguzi. Tunaendelea na upelelezi juu ya kesi ya mauaji dhidi ya watuhumiwa. Tumeshasafirisha mwili kwenda kwenye halmashauri ya Hospitali ya Mulago ambako mtaalamu ya pathologist atafanya postmortem kabla mwili kukabidhiwa kwa ndugu" Alisema hayo kamanda wa polisi Benson".
Inasemakana mtoto Anita alifariki wiki 2 zilizopita. 
Kiongozi wa Usharika wa Umoja wa Wachungaji wa Luweero. Mchungaji Morris Kigongo ameelezea kwamba alikuwa hamtambui mchungaji Viola na wala hakuwa katika orodha ya wachungaji waliopo katika wilaya hiyo. 

Akaongeza kwa kusema kuwa Viola alikuwa akitenda vitendo vya kichawi na sio ukristo.

No comments