Mchungaji akamatwa akifanya maombi na wanawake 7 wakiwa uchi nyumbani kwake


Mchungaji mmoja na waumini wake saba wa kike wamekamatwa nchini Uganda kwenye nyumba moja walimokuwa wakifanya maombi yao bila kuvaa nguo hata moja. Wanawake hao wanasemekana wamekuwa wakifanya maombi hayo wakiwa uchi bila hata nguo za ndani mbele ya mchungaji wao.Tukio hilo lililotokea Siku ya Jumanne Oktoba 2.

Kwa mujibu wa Daily Mirror, Waumini hao pamoja na mchungaji wao ambao ni waumini wa kanisa la Full Gospel walikamatwa na maafisa wa polisi kwenye nyumba moja eneo la Rukiga. Kutokana na mkuu wa wilaya hiyo Emmy Ngabirano, alisema kuwa ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kuwa wanawake hao 7 wote walikuwa wameolewa na wapo katika ndoa.

Ngabirano alishtumu kitendo hicho huku akidokeza kuwa kanisa walilodai kuwa wanachama wake halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria. "Tunaheshimu uhuru wa kuabudu lakini watu wanafaa kufuata sheria zilizopo za kuendesha kanisa na mojawapo ya sheria hizo ni liwe limesajiliwa. Waliokamatwa wanaendesha mikutano haramu nyumbani kwa mtu ambapo wanadai kuwa kanisa walipopatikana wakiwa uchi," Alisema Ngabarino. 

Kwa mujibu wa ripoti zilizotufikia InjiliOnline wanawake hao hawakuwa tu wakifanya maombi wakiwa uchi bali pia walitoweka majumbani mwao kwa muda wiki kadhaa.

Source: Daily Monitor

No comments