Historia ya Ukristo


 Ukristo ni dini inayofanywa sana Duniani (Dini kubwa Duniani) Ikiwa na wafuasi/waumini zaidi ya bilioni 2.4 Duniani kote. Kitovu kikuu cha imani ya kikristo kinahusishwa na kuzaliwa, maisha, kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo. Waumini wa kikristo wanasisitiza na kuweka mkazo juu ya Yesu ni Mwana wa Mungu, Mwokozi wa Binadamu, ambaye kuja kwake kama Masihi (Kristo) kulitabiriwa katika Agano la Kale la Biblia, na kuandikwa katika Agano Jipya la Biblia.

Ukristo ulikua kutoka kwa Dini ya kiyahudi na ulianza kama Dini ya pili ya Hekalu la Kiyahudi katikati ya karne ya 1, katika jimbo la kirumi la Yudea. Mitume wa Yesu na wafuasi wao, walitapakaa na kueneza ukristo katika maeneo ya Syria, Ulaya, Anatolia, Mesopotamia, Transcaucasia, Misri, Ethiopia, na Asia licha ya mateso makali ya awali. 
Wakati ukristo ukianza na kikundi kidogo cha wafuasi. Wanahistoria wengi wanaona kuenea na kupitishwa kwa Dini ya Kikristo ulimwenguni kote ni kama moja ya ujumbe wa kiroho wenye mafanikio zaidi katika historia ya Dini na historia ya Binadamu. 
Imani ya kikristo imejengwa katika misingi ya mawazo ambayo inaamini katika 'Monotheistic' yaani imani katika Mungu mmoja tu. Aliumba mbingu na nchi. Uungu huu wa Mungu unasehemu tatu: Baba (Mungu mwenyewe), Mwana ( Yesu Kristo) na Roho Mtakatifu.
Kiini cha ukristo kinazunguka maisha, kifo na hasa imani katika ufufuo wa Yesu. Wakristo wanaamini Mungu alimtuma mwanawe Yesu, masihi, kuokoa ulimwengu.
Wao huamini alisulubiwa msalabani ili atoe msamaha wa dhambi na kufufuliwa siku ya tatu baada ya kifo chake kabla ya kupaa mbinguni.
Wakristo wanasisitiza kwamba Yesu Atarudi duniani tena katika kile kinachojulikana kama Ujio wa pili. 
Wakristo wanaamini katika Biblia Takatifu ambayo ndani yake kumejaa mafundisho na maelekezo jinsi wakristo wanapaswa kuishi. 
Sikukuu muhimu katika dini ya ukristo ni Krismasi (Ambayo inaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu) na Pasaka (Ambayo inakumbuka kufufuka kwa Yesu) 
NB: Msalaba ni alama/ishara ya Ukristo.

Cc: Source; www.history.com
Edited by @tabasamu_tz

No comments