Pastor Safari Paul: Sound Mbaya Kwenye Ibada hukata Upako

Kati ya vitu muhimu sana kwenye Ibada ni Sound.  NI bora kuwa kwenye Ibada ambayo haina vyombo kuliko Ibada yenye vyombo na sound ni mbaya. "Amesema hayo Pastor Safari Paul, Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram".
Aliongeza, Huwa ninashindwa kuabudu ninapokuwa kwenye Ibada ambayo sound inavurugu, vyombo juu, sauti za waimbaji juu basi inakuwa mashindano. - Kama sound ni mbaya sana au inavurugu, huwavuruga pia watumiaji wa vyombo hivyo. - Kama sound ni mbaya huwaumiza wasikilizaji na kama ni Ibada watu hushindwa kuabudu vizuri na mawazo yao yanaenda kwenye hiyo sound mbaya.
USHAURI - Kwa wale wanaoandaa events wekeza Kwanza kwenye sound alafu mengine yatafuata. Watu wengi huweka pesa kwenye mambo mengine alafu wanaweka bajeti mdogo kwenye sound. Mwisho wasiku vyombo kama havifanyi kazi vizuri lengo halitafikiwa. - Kwa Wachungaji na wote wenye huduma,  wasaidieni mafundi mitambo wenu wajifunze sound. Makanisa, au wenye vyombo huingia hasara maana amplifier na speaker zinaungua kila mara. - Wapiga vyombo, waimbaji tutoe ushirikiano kwa mafundi mitambo. Usitake wewe peke yako usikike. NI ubinafsi kutaka wewe ndo usikike saana kiliko wengine.
Mafundi mitambo tamani kujifunza zaidi kwa wanaofanya vizuri katika eneo hili.  Soundi nzuri haiji kwa maombi bali ni kwa ujuzi. Maombi hukusaidia upate upako wa kufanya kazi yako vizuri.
#NisalamandaniyaYesu

No comments