Nabii Daniel Shillah: Toka utotoni nilikuwa mtu wa miujiza: Bado nipo na Yesu sijakata nae tamaa


Kiongozi wa Huduma ya Bethel International Ministry Nabii Daniel Daniel Shillah ameonyesha msingi na mzizi wake wa kumtumikia Mungu toka yupo utotoni. Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram Nabii Shillah ameshirikisha picha zake kuonyesha kuwa huduma na miujiza anayoifanya sasa hivi alikuwa akiifanya pia miaka mingi iliyopita toka alipokuwa mtoto mdogo. 


"Nikiwaambia mimi toka utotoni ni mtu wa miujiza mnanibishiaπŸ˜‚ , yani hapo nakumbuka nilikuwa nagonga maombi shule yote kimyaa 😁, Alafu sasa natumiaga hata lisaa yani nkitoka hapo kuna wengine wanannimind 😁😁😁😁 , Nilivurugwa sana yani kuna Muda napiga kifaransa,Kiswahili nanena kwaruga yaani inshort tafuta niliosoma nao form 1 ,nilikua NAGONGA TU SINA HABARI πŸ˜‚ , Hadi Leo nipo na Yesu sijakata nae tamaa ila tunao watu, watumishi ambao pengine walishamuacha Yesu au yamkini unaangalia posti hii na unampango wa kumuacha Yesu pokea UPAKO WA KUKAA NA YESU BILA KUMUACHA #Receive
.
#HIV_specialist ".


"Nakumbuka hapa nilikuwa nafokea walimu na mkurugenzi nilikuwa nasema “NASEMA FUNIKA MACHO TUOMBE HATA KAMA WEWE NI MWALIMU AU KIONGOZI YEYOTE πŸ˜‚πŸ™πŸ½”
.
Sasa hapo kwenye Shati nilijiandika DANI πŸ˜†πŸ˜’ TULIAMBIWA KILA MTU AANDIKE JINA LAKE KWA UZI ILI KUPUNGUZA WIZI WA MASHATI, dah ila shule noma sana 😁🀣 .
Alafu kwenye maombi haya kuna mwanafunzi alikuwa anatokwa na damu sehemu za siri (sitomtaja jina) Alipona #CONNECT #JIAMBATANISHE ". Aliandika hayo kupitia kurasa yake ya Instagram.

Nabii Shillah ambaye amejizolea umaarufu zaidi katika mitandao ya kijamii kwa namna ambayo amekuwa akihudumia watu na kutenda miujiza, hali iliyopelekea baadhi ya watu kuwa na maswali mengi juu yake na huduma ambayo amekuwa akiifanya, maswali kama ametokea wapi, alianza huduma wapi, amepata wapi nguvu za kutenda miujiza. Lakini leo maswali hao yameweza kujibiwa kwa picha dhahiri kwamba yeye ni mtumishi wa Mungu kweli na amekuwa na karama ya kinabii ambayo Mungu ameweka ndani yake toka utotoni.

Tazama Picha zaidi za Nabii Shillah akifanya kazi ya Mungu.Twitter : @InjiliOnline
Facebook : @InjiliOnline
Google + : @InjiliOnline
Instagram: @InjiliOnline
Mobile: +255714790330

No comments