Uzuri wa sura wamfanya Emmanuel Mbasha kuombwa kuwa Baba wa Kiroho


Mfanyabiashara na Muimbaji muziki wa Injili Tanzania Emmanuel Mbasha ambaye amekuwa akifuatiliwa sana hasa juu ya mtindo wake wa maisha, namna ambavyo amekuwa akijiweka wakati wote katika hali ya Utanashati, na kupelekea watu wengi  hasa vijana kumtazama kama mtu wa mfano kwenye masuala ya kuvaa na kuwa smart.

Emmanuel Mbasha ambaye amejizolea umaarufu katika nyanja hiyo ya kuwa nadhifu hali hiyo imemfanya mmoja wa wasanii wa nyimbo za Injili kuweza kumuomba Emmanuel Mbasha kuwa Baba yao wa kiroho kwa kuwa amewazidi vitu vingi kulinganisha wasanii wengine wa Muziki wa Injili.
Kupitia Group moja la Mtandao wa WhatsApp linaloitwa CHAMUITA. Msanii huyo aliweka  wazi hisia zake na kuandika ujumbe huu kwa Mbasha.

"Nimefurahi kumuona muimbaji mwenye muonekano mzuri na kibali kikubwa kuliko waimbaji wooote wa injili, Prophet Emmanuel Mbasha, Major One. Ninalo ombi moja kwako baba Mbasha, kwa niaba ya waimbaji wooto waliyoko humu na walioko nje ya group hili ningekuomba uwe baba yetu na utulee sisi wanao, Maana kwa kweli umetuzidi wooote kwa mambo mengi, kifedha, kupiga pamba, exposure, umaarufu, uzuri wa uso na umbo, mpaka kuwa na comment nyiiiiiiingi Instagram. baba mbasha naomba utukubalie ombi letu sisi sote tulioko hapa na waimbaji wote walioko nje ya group hili tunaomba utulee baba, kwa maana kuna mengi sana tunahitaji kujifunza toka kwako.
Karibu baba ulifikilie ombi letu.".

Baada ya kupokea Ujumbe Mbasha aliamua kushirikisha pia kwa Followers wake Instagram kwa Kukubali Ombi la msanii huyo.
 Yafutayo ni baadhi ya maoni juu ya ombi la msanii huyo kwa Mbasha.

 • @adimora_Mbinguni hatuendi kwa umaarufu wala uzuri, wasikutie ndimu nadhan unalijua hilo mtumishi , naona huyo aliyeandika hivyo atakua alionja beer Kidogo, sio akili za watu waliokoka
 • @mwanza_home_of_deliveryKumbe Ukiwa Na Comments, nyingi Instagram na Uso Mzuri Unaweza Kuwa Baba Wa Kiroho.... nimecheka sana.. kwahio hapo mzee baba unawanyoosha Uongo... Haya HANDSOME MUIMBA INJILI WALEE WANAO..
 • lilian_seboimandaMungu akuinue zaidi ufanye kazi ya Mungu..uliyoitiwa kwa nguvu 🙏
 • @shillah_tzMimi hapo kwenye Uzuri wa Sura na umbo, pamba kali ndiyo pameniacha na swali. Je, hii ina "exposure" gani katika mambo ya Kiroho? Kwamba wanataka uwe "BABA YAO WA KIROHO au KIONGOZI" kwa ajili ya hayo pia? Mungu akubariki kaka. @e.mbasha
 • @financial_freedom18Yaani mwanaume unasifiwa mzuri Eti wa uso😰😰😰😰 unaona raha kabisa, hapo ungeambiwa u mrembo ungeleta hapa pia, hivi wanaume wa miaka hii mmekuaje lakini?? Ama kweli Madam alikua amebeba gunia la misumari kwenye upara.
 • @christinashushoHahahahaha hahahahaaaa hahahahaaaa 😀😀😀😀😀 @e.mbasha yaani kakangu weye una mambo. Sifa zilizotajwa hapo juu zote nime zipenda 😀😀😀😀😀
 • @barnabaclasicHapo kwenye Uzuri wa uso na umbo 😂
 • @zulphakimaro7909Nakwel hizo c akili za watu waliookoka... Mbingun hatuend kwa umaarufu muonekamo mzuri cjui utajir cjui umbo sura eti adi comments nyingi Instagram khaaa walokole waleo ni hatwariiii khaaa kwel kwa hzo sifa Aya kawe baba wakiroho
 • @lilianflikleyProphet tena..?
 • @zulphakimaro7909Kaka una masifa ww yan nyie ndo mnafanya watu wasimuamin Yesu kwa upuuzi wenu kama huuu cjui ata umeenda kuwaje
 • @adela_totolakisukumaNice one tusimlaumu sana aliye andika huo ujumbe kila mtu anupeo wake wakuandika apo yeye ndiyo aliona ameandika vizuri mimi simlaumu ombi lake limetoka moyoni 👌🏿
 • @zulphakimaro7909Ata ukifuta comment haisaidii ila ukweli nmeshakupa.. Ukokeni acheni usanii#idiot
TAZAMA PICHA ZAIDI YA MBASHA HAPA


NINI MAONI JUU YA SUALA HII? JE MBASHA ANAFAA KUWA BABA WA KIROHO KWASABABU YA UZURI WA USO?

No comments