JIM CAVIEZEL STAR WA HOLLYWOOD ALIYEAMUA KUOKOKA BAADA YA KUIGIZA KAMA YESU.


Huyu ni Jim Caviezel, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa duniani kwa filamu zake za mapigano ya kiutaalamu na ujuzi wake hasa akicheza kama adui.

Anasema kwanza hakutaka kabisa kuigiza filamu ya "The Passion of the Christ", baada ya kupewa offer hiyo na Mel Gibson ambaye ndiye muongozaji wa filamu hii.

Lakini baadaye alikubali, na mambo yaliyomtokea wakati wa uandaaji, wakati wa kujifunza lugha ya kiebrania, maana ilibidi watumie lugha hiyo, kuleta uhalisia, ni mambo yaliyombadilisha kabisa.

Anasema jinsi alivyokuwa akishutumiwa kama Yesu, wakimkebehi, na hata wakati akisulubiwa na kupigwa, alihisi uchungu sana na ukawa wasaa mzuri wa kufikiri kuhusu maisha ya dhambi aliyokua akiishi.

Kuna wakati wale askari walikosea na walimpiga kweli, maana walikua watu wa Roma, hawajui kingereza hivyo mis-communication, zilitokea mara kadhaa, na aliumia kweli.

Kubwa kuliko yote ni alipokua anaelekea kuwekwa msalabani, pale kilimani, alipatwa na hali isiyo ya kawaida, alipoteza fahamu, lakini baadaye waliendelea, na hata alipoambiwa basi aache , alisisitiza kumalizia, maana aliona Mungu ameamua kumtumia kwa njia hiyo.

Mara baada ya movie kuigizwa, aliumwa sana, na pia baada ya kupona alikataa kuigiza movie zozote akifanya mapenzi au mauji ya kikatili, kama alivyowahi kufanya kabla.

Ametengeneza Biblia ya Sauti, kurahisisha watu kulijua Neno, pia amekua akizunguka kuhamasisha watu kumtumikia Mungu zaidi, na hata mahojiano mbali mbali amekua akikiri kuwa mtumishi na Yuko tayari kufa kwaajili ya Injili.

The Passion of the Christ, imetoka mwaka 2004, ni filamu ya mateso ya Yesu, yenye mafunuo ya hali ya juu, produced and directed by Mel Gibson.


No comments