Itambue Namna Ya Kuenenda Sawa na Mungu


Ili kuweza kuenenda sawa na Mungu, ni sharti mwanzo tuelewe “makosa” yako wapi. Jibu ni dhambi. “Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la! hata mmoja” (Zaburi 14:3). Tumeasi kwa kukeuka amri za Mungu; Tumekuwa “kama kondoo tumepotea” (Isaya 53:6).

Habari mbaya ni kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. “Roho ile itendayo dhambi itakufa” (Ezekieli 18:4). Habari njema ni kuwa Mungu mwenye upendo alitutafuta ili akatuletee wokovu. Yesu aliapa ya kwamba madhumuni yake ilikuwa ni “kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10), na akatamka madhumuni yake yakuwa imekamilika, wakati alipokufa msalabani, kwa maneno “imekwisha” (Yohana 19:30).

Kuwa na uhusiano wa sawa na Mungu yaanza kwa kutambua dhambi yako. Halafu ifwatilie hali ya kukiri dhambi hiyo mbele za Mungu kwa kunyenyekea (Isaya 57:15) na ujasiri wa kuiacha dhambi hiyo. “Kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10).

Toba hii ni sharti iambatane na imani. Kwa hali ya kipekee, imani yakuwa kifo cha Yesu cha kujitoa na ufufuo wa kiajabu inamwidhinisha kuwa mwokozi wako. “Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka” (Warumi 10:9). Vifungu (vitabu) vyengine vinazungumzia umuhimu wa imani, kama vile Yohana 20:27; Matendo 16:31; Wagalatia 2:16; 3:11, 26; na Waefeso 2:8.

Kuenenda sawa na Mungu ni jinsi utakavyo itikia kwa kile ambacho Mungu ametenda kwa niaba yako. Alituma mkombozi, Alitoa dhabihu ya ondoleo la dhambi yako (Yohana 1:29), na anakupea ahadi: “Na itakuwa kila atakaye liita jina la Bwana ataokolewa” (Matendo 2:21).

Maelezo mazuri kuhusu Toba na Msamaha ni lile fumbo la mwana mpotevu (Luka 15:11-32). Mvulana huyo mdogo alitapanya urithi aliopewa na babake kwa njia ya uasherati (aya13). Alipotambua makosa yake, aliamua kurudi nyumbani (aya18). Alidhani hangeliweza kuhesabika tena kama mwana (aya19), lakini haikuwa kweli. Babake alipendezwa na kurudi kwake mtoto huyo mwasi, zaidi kuliko mwanzo (aya20), kila kitu alisamehewa na sherehe zikafuatilia (aya24).

Mungu ni mwema kwa kutimiza ahadi zake, hata kwa ahadi ya kusamehe. “Bwana yu karibu na waliopondeka roho huwaokoa” (Zaburi 34:18).

Kama unataka kuenenda sawa na Mungu, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka yakwamba kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile, haitaweza kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kwa kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo aliichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha- karama ya uzima wa milele! Amina!”


No comments